Mwanachama ataweza kukopa mkopo huu bila akiba maalumu lakini ataweka dhamana isiyohamishika kwa riba ya asilimia kumi na moja (11%) na muda wa marejesho itakuwa miezi thelathini na sita (36). Ili mwanachama aweze kukopa mkopo huu atapaswa kuwa na;
- Biashara rasmi iliyosajiliwa BRELLA
- Namba ya Mlipa Kodi
- Leseni Hai ya Biashara
- Nakala ya hesabu za biashara yake (Financial Statement)
- Taarifa zake za kibenki (Bank Statement)
- Kusajili dhamana yake kwenye mamlaka husika
Aidha mwanachama atarejesha mkopo huu kupitia biashara yake kwa njia ya “Standing Instruction” na mshahara